Breaking News

Wanafunzi wawili waleta mapinduzi ya kimtandao!



Peter Moris (20) na Issambi Mwashibanda (19) ni wanafunzi wa kozi ya muda mfupi ya computer katika chuo cha Grace College kilichopo jijini Mbeya. Ni wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka 2017.
Peter na Issambi ni wanafunzi wenye malengo ya kuwasaidia wanafunzi wenzao waliopo shuleni katika kusoma na upatikanaji wa materials za kusomea kama notes, past papers na video za masomo mbalimbali.
Peter na Issambi waliamua kutengeneza website yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi wenzao katika upatikanaji wa notes na past papers pamoja na kuwawezesha wanafunzi kufanya group discussions kupitia website hiyo. Pia Peter na Issa waliamua kuanzisha vipindi vya youtube ambavyo vinakuwa na videos za masomo mbalimbali ili kurahisisha usomaji kupitia mtandao.
Pamoja na changamoto nyingi wanazopitia ikiwamo ukosefu wa vifaa vya kutengenezea website hiyo na urushaji wa vipindi vyao mtandanoni, Peter na Issa wameweza kutumia vifaa vya chuoni kwao na kufanikisha kutengeneza baadhi ya vipindi youtube pamoja na kuanza kutengeneza website ambayo mpaka sasa imekamilika kwa asilimia 80%.
Vijana hawa wameonesha ubunifu na uwezo wao katika kutumia teknolojia kuonesha vipaji vyao na kujaribu kutengeneza njia za kutatua matatizo yaliopo kwenye jamii.

Hii ni video mojawapo inayopatikana katika youtube channel yao.



Kwa maelezo zaidi kuhusu vijana hawa contacts: paxcoded@gmail.com au 0768825770

No comments