Breaking News

Jeshi la Polisi Manyara linamshikilia Mbunge Mary Nagu

Leo March 7, 2018 Mbunge wa Jimbo la Hanang, mkoani Manyara Dkt Mary Nagu(CCM) na mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo waanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo kwa amri ya Mkuu wa wilaya hiyo kutokana na sababu ya  kushindwa kuelewana kiutendaji.
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya Sarah Msafiri ameeleza kuwa ameagiza kukamatwa kwa Mbunge huyo baada ya kuchoka kumvumilia kutokana na kauli anazozitoa kwenye mikutano yake na wananchi akihamasisha wasishiriki shughuli za maendeleo.
Pia amemtuhumu Mbunge huyo kuwataka wananchi wasishirikiane naye jambo ambalo alidai ni sawa na kuwataka wananchi wasishirikiane na serikali kwa sababu yeye anasimama kama serikali

1 comment:

  1. JTG Marriott Hotel & Casino - Hollywood, LA
    JTG Marriott 사천 출장안마 Hotel & Casino locations, rates, amenities: 안양 출장샵 expert Hollywood 속초 출장마사지 research, only at Hotel 밀양 출장안마 and Travel Index. Book 평택 출장샵 online or call now!

    ReplyDelete