Breaking News

Msimamo wa EPL, Chelsea ikiiua ManUnited, Arsenal wakiondoka vichwa chini Etihad

November 5 2017 Ligi Kuu England iliendelea kwa michezo kadhaa kuchezwa ikiwemo big match za Chelsea dhidi ya Man Unitediliyomalizika kwa Chelsea kupata ushindi wa goli 1-0, goli likifungwa na Alvaro Moratadakika ya 55 kwa kichwa.

Big Match nyingine ilichezwa katika uwanja wa Etihad kati ya wenyeji Man City wakicheza dhidi ya Arsenal, game ambayo ilimalizika kwa Man City kupata ushindi wa magoli 3-1, magoli ya Man City yakifungwa na Kelvin De Bruynedakika ya 19, Sergio Aguero kwa penati dakika ya 50 na Gabriel Jusus dakika ya 75.

Arsenal wakipata la kufutia machozi kutoka kwa Alexandre Lacazette dakika ya 65, ushindi huo sasa umeifanya Man Citykuenelea kuwa kileleni mwa msimamo wa EPLkwa kuwa na point 31 wakati Chelsea wakiwa nafasi ya nne kwa kuwa na point 22.

Matokeo ya game zote za EPL zilizochezwa November 5 2017.

Msimamo wa EPL ulivyo kwa sasa

No comments