MBEYA CITY 0 - 1 SIMBA
Simba wamerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila, mechi iliyopingwa kwenye dimba la Sokoine
Baada ya ushindi huo Simba wanafanikiwa kufikisha alama 19 katika mechi 9, wameshinda mechi 5 na sare mechi 4 huku wakiwa sawa na Waoka Mikate wa mbele
Dakika ya 7 Shiza Kichuya anaipatia goli Simba kufuatia makosa ya walinzi wa Mbeya City ya kumuacha wiga huyo wakizani ameotea, baada ya goli hilo mpira ulionekana kupooza kutokana na timu zote mbili kucheza kwa tahadhari kubwa.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku wenyeji wakionekana kutaka kusawazisha goli lakini safu ya ulinzi ya Simba iliyokuwa chini ya Juuko Murshid na James Kotei ilikuwa kikwazo kwa wagonga nyundo hao kushindwa kupata goli.
No comments