Breaking News

NEWS:MANCHESTER CITY V ARSENAL: WENGER ANA KIBARUA KIGUMU CHA KUISIMAMISHA CITY TISHIO

Arsenal wana kibarua kizito cha kuukomesha mwanzo mzuri wa Manchester City watakaposafiri kwenda Etihad Jumapili leo.

Mwanzo wa kishindo wa City umewawezesha kucheza mechi 16 za awali katika michuano yote bila kufungwa na mwendo huo umeamsha mjadala kama wanaweza kumaliza kampeni zote bila kufungwa.

Timu ya mwisho kufanya hivyo Ligi Kuu Uingereza walikuwa wapinzani wao wa wikiendi hii, Arsenal 2003/04, ambapo pia Gunners ndiyo timu ya mwisho kuwafunga vijana wa Pep Guardiola kwenye Kombe la FA nusu fainali mwezi Aprili.

No comments