Breaking News

TIZI LA SIMBA LAMTISHA KOCHA WA YANGA LWANDAMILA


Kikosi cha Simba kimewasili Visiwani Zanazibar tayari kwa kambi ya wiki moja kwa ajili ya kuwakabili watani zao wa jadi Yanga, lakini kocha wa timu hiyo Joseph Omog, amesema anakwenda kwenye mchezo huo akijivunia rekodi yake nzuri ambayo anaamini itambeba na kupata ushindi Jumamosi.

Omog ameiambia Goal, anatambua kuwa Yanga ni timu nzuri lakini kikosi chake ni bora zaidi ya ya mabingwa hao watetezi ambao wanalifukuzia taji la nne mfululizo la ligi hiyo.

"Nimeifunga Yanga mara mbili na kutoka sare mechi moja katika mechi sita nilizocheza nao nikiwa kocha wa Simba, kwahiyo najivunia rekodi hiyo ambayo naamini itanibeba na kupata matokeo mazuri katika mechi ya Jumamosi na hata mechi nyingine za ligi na michuano mengine," amesema Omog.

Kocha huyo amesema kambi yao ya Zanzibar, itakuwa ni maalumu kwa ajili ya kuwaweka sawa wachezaji wake na kuwakumbusha yale mambo muhimu yatakao wasaidia kupata ushindi na kujilinda ili wasiweze kupoteza mchezo.

Amesema anawajua Yanga, lakini siyo timu tishio kwake kutokana na ubora wa safu ya ushambuliaji na ulinzi imara ambao ameuandaa dhdi ya mshambuliaji Ibrahim Ajibu anayeonekana kuwa moto wa kuotea mbali kutokana na aina ya mabao aliyofunga katika mechi zilizopita.

Mechi ambazo Omog ameshinda dhidi ya Yanga ni ya Ligi Kuu Bara msimu uliopita Simba ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-0. Omog akaiongoza tena Simba kuifunga Yanga kwa penalti 4-2 kwenye Kombe la Mapinduzi, kabla ya kuibuka tena na ushindi wa penalti 5-4 kwenye Ngao ya Jamii msimu huu.

No comments