Breaking News

KOEMANI AFUNGASHIWA VILAGO EVERTON

Kibarua cha Mholanzi huyo kimefikia kikomo miezi 16 tangu akabidhiwe mikoba ya kuinoa timu hio

Everton wameachana na Ronald Koeman baada ya kipigo cha 5-2 mikononi mwa Arsenal walichokipata Jumapili, ambacho kimeiacha timu hio na ushindi katika mechi mbili tu tangu msimu uanze na ikishuka katika nafasi za timu zenye hati hati ya kushuka daraja.

Koeman alipewa fungu kubwa la usajili wa wachezaji ambapo Everton ilitumia kiasi cha Paundi 142 katika usajili wa wachezaji wapya.

Lakini klabu hiyo ya Merseyside imeshindwa kufanya vyema na licha uonyesha dalili za mapema za kufanya vyema. Waliambulia kushinda mara moja tu katika ligi tangu walipopate sare ya 1-1 dhidi ya Manchester City katika mchezo wao wa pili wa msimu.

Walionyesha kiwango kizuri walipopambana na kupata sare dhidi ya  Brighton and Hove Albion mnamo Oktoba 15, lakini matokeo mazuri yalishindwa kuendelea na kuipa timu mafanikio. 

Na matokeo ya Jumapili ilikua ni pigo la mwisho kwa  Koeman, ambaye anaondoka miezi zaidi ya 16 baada ya kuondoka Southampton na kujiunga na Goodison Park.

No comments