Breaking News

Jinsi watu wanavotengeneza pesa kupitia YOUTUBE.


Mtandao wa youtube ni moja ya mitandao mikubwa  duniani ambao unafukuzana na google kwa idadi ya watumiaji. Mtandao huu umekuwa ukitumika katika kuelimisha na pia entertainment. Ukiachana na matumizi hayo, youtube kwa sasa imechukuwa nafasi kwa kasi kutokana na uwezo wa kutengeneza ajira kwa vijana wengi. 
Mtandao wa youtube ukishirikiana na kampuni ya adsense wanamlipa kila mmiliki wa youtube chanel kutokana na views zilizofikishwa kwenye video. Pesa hio inalipwa kutokana na matangazo yatayooneshwa na youtube kupitia video iliowekwa. 
Baadhi ya masharti yaliowekwa na youtube iliuweze kulipwa ni haya:
- ni lazima uwe na youtube channel 
- ni lazima uwe una subscribers kuanzia 1000 
- ni lazima uwe na adsense account.
- ni lazima uwe na bank account iliounganishwa na Mastacard, Visa, Maestro au PayPal.
Baada ya kutimiza masharti hayo unaweza kujiunga na kujitengenezea pesa kutokana na views utazozipata kwa kila video utayoiweka katika channel yako.

No comments