PICHA 4: Matokeo ya Europa League Nov 2, Evra akimpiga shabiki kabla ya game

Usiku wa November 2 2017 game 24 za michuano ya UEFA Europa League zilichezwa barani Ulaya ikiwa ni siku moja imepita toka zichezwe game za round ya nne za michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2017/2017.

Game zote 24 zimechezwa na kuona baadhi ya timu zikiondoka na ushindi na nyingine zikitoka uwanjani vichwa chini, tukio kubwa lililosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na Europa Leagu ni kuhusiana na beki wa zamani wa Man United raia wa Ufaransa ambaye kwa sasa anaichezea Olympique Marseille ya Ufaransa Patrice Evra.

Patrice Evra usiku huo ameingia katika kitabu cha kumbukumbu mbaya baada ya kuoneshwa kadi nyekundu kabla ya game kuanza wakiwa wanafanya warm up kabla ya mchezo dhidi ya Vitoria Guimaraesuliyomalizika kwa Marseille, kupoteza kwa goli 1-0 lililofungwa na Christopher Hurtado dakika ya 80.

Evra alioneshwa kadi baada ya kufikia uamuzi wa kumpiga shabiki wa Marseilleambaye inadaiwa walipishana kauli kabla ya game hiyo iliyochezwa Ureno, Evrasasa anakuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Europa League kuoneshwa kadi nyekundu kabla ya game kuanza
Tunashukuru kwa habari za uhakika. website nzuri sana hii
ReplyDelete