News:Soka La Neymar Kwaheri
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Brazili ataikosa mechi ya Ijumaa dhidi ya Nice baada ya kupata kadi mbili za njano
Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Neymar atatumikia adhabu ya kukosa mechi moja kufuatia kadi nyekundu aliyopata dhidi ya Marseille Jumapili.
Baada ya kupata kadi yake ya kwanza nyekundu tangu ajiunge na miamba hao wa Ligue 1 kutoka Barcelona kwa uhamisho wa rekodi, Neymar atalazimika kuiangalia kutokea jukwaani mechi ya PSG dhidi ya Nice Ijumaa.
Mbrazili huyo alitolewa dakika za mwisho katika sare ya 2-2 kwenye Le Classique baada ya kusukumana na Lucas Ocampos, ambaye huenda alikuza tukio hilo.
Ilikuwa ni kadi ya pili kwa Neymar ya njano ndani ya dakika tatu, lakini Edinson Cavani alifanikiwa kuwapatia vinara hao wa Ligue 1 PSG pointi moja kwa mpira wa adhabu aliopiga dakika za lala salama.
Kwa update icikose kutembelea hapa.
No comments