#News:Polisi 350 Kumwagwa Uwanja Wa Uhuru
Licha ya udogo wa Uwanja wa Uhuru, Polisi zaidi ya 350 watakuwepo kuhakikisha usalama unakwenda vizuri katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom baina ya watani wa jadi Yanga na Simba.
Utaratibu wa kuingia uwanjani uko hivi;
Mageti yatakayotumika ni mawili, yote yenye mfumo wa tiketi za kielektroniki. Mageti hayo yana jumla ya milango midogo 20 ya kuingilia hivyo kutoa fursa ya watu wengi kuingia ndani ya muda mfupi.
Mageti mengine mawili yaliyopo mbele ya uwanja wa Uhuru, yatatumika kwa mashabiki waliokata tiketi za VIP.
Kwa wale wa mzunguko, wataingilia geti la nyuma ya uwanja wa uhuru (in door), ambalo linaelekea kwenye uwanja wa ndani wa Taifa.
Geti jingine ni lile la kuingilia mashabiki wa Yanga la Uwanja wa Taifa. Mageti hayo mawili yatatumiwa na mashabiki zaidi ya 20,000 watakaokata tiketi za mzunguko.
Uongozi wa Yanga umewataka mashabiki wake 12,000 wanaoingia kwenye mechi hiyo wawahi mapema kuingia uwanjani.
Mchezo huo utaanza saa kumi kamili jioni.
No comments