News;David Unsworth Kurithi Mikoba Ya Koeman
Majabu ya Everton ya nchini Uingereza inayodhaminiwa na kampuni ya kubashiri matokeo ya SportPesa hii leo imemthibitisha, David Unsworth kurithi kwa muda mikoba iliyoachwa na aliyekuwa meneja wa timu hiyo Ronald Koeman ambaye alitimuliwa kazi baada ya kuiongoza kwa miezi 16 ndani ya mkataba wake wa miaka mitatu
Koeman mwenye umri wa miaka 54, ameachishwa kazi siku ya Jumatatu hukua akiiacha Everton ikiwa ya tatu kutoka chini ya msimamo wa ligi ya Uingereza baada ya kushinda michezo miwili pekee kati ya 13 iliyocheza.
Uwamuzi wa kuachishwa kazi kwa Koeman umefanywa na tajiri Farhad Moshiri ambaye ni mbia mkuu ndani ya klabu hiyo na kufika kwa mwenyekiti, Bill Kenwright kisha mtendaji mkuu Robert Elstone akamuambia Koeman juu ya hatima ya kibarua chake baada ya matokeo ya 5-2 dhidi ya Arsenal.
No comments