Breaking News

Breaking:Ronaldo Atangazwa Na Fifa Mchezaji Bora

Nyota wa Real Madrid ameshinda tuzo hiyo kwa mwakwa wa pili mfululizo baada ya kuwaongoza Blancos kutwaa Liga na Ligi ya Mabingwa

Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ametajwa kuwa mchezaji bora wa FIFA wa mwaka upande wa wanaume 2016-17.

Ronaldo ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo, baada ya kufanikiwa kuwashinda Neymar na Lionel Messi katika sherehe za tuzo hiyo mjini London.

Mreno huyo, 32, alipata mafanikio makubwa katika kampeni za 2016-17 kwani aliwaongoza Blancos kutwaa taji la La Liga na Ligi ya Mabingwa, ikiwa ni pamoja na kufunga mabao mawili fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Juventus.

Messi, kwa upande wake alifunga magoli 54 katika mechi 52 kwenye michuano yote msimu uliopita, lakini alifanikiwa kutia taji moja tu mikononi mwake, Copa del Rey akiwa na Barca - na ni mataji tu ya Madrid yaliyomwezesha nyota wao kutwaa tuzo hiyo maarufu.

"Asanteni sana, kwa wale wote walionipigia kura. Sina budi pia kuwataja Leo na Neymar kwa kuwa hapa," Ronaldo alisema baada ya kupokea tuzo.

"Real Madrid, Kocha, mashabiki na rais - kwa ushirikiano wenu wote kipindi cha mwaka mzima, nawashukuru sana.

"Nimefurahi sana kutwaa tuzo hii mfululizo. Huu ni wakati mzuri sana kwangu. Shukrani nyingi sana kwa mashabiki kote duniani kwa kuniunga mkono. Nashukuru sana kwa hilo.

"Inapendeza kuwa hapa na wachezaji hawa wakubwa, na nimefurahia sana, asanteni sana."

No comments