Breaking News

AJIBU:NIKIIFUNGA SIMBA NA KWENDA KWA MASHABIKI WAKE

STAA wa Yanga, Ibrahim Ajibu, amesema mechi yao ijayo dhidi ya Simba itakuwa ngumu, lakini atahakikisha anaipambania timu yake ipate ushindi utakaowaweka sehemu nzuri.

 

Ajibu ameyasema hayo zikiwa zimebaki siku chache kabla ya timu hizo hazijapambana Juma­mosi hii kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa katika Uwanja wa Uhuru, Dar.

 

Ajibu aliongeza kuwa, kazi yake ni kufunga, hivyo atapambana kuhakikisha anafunga na akifani­kiwa kufanya hivyo, basi atashangilia kama kawaida.

 

“Unajua mechi hii haiwezi kuta­birika, lakini yeyote atakaye­zichanga vizuri karata zake ndiye atakayeibuka na ushindi.

 

“Binafsi nitaipambania timu yangu ishinde ikiwemo mimi mwenyewe kufunga bao, na ikitokea kweli nimefunga nitashangilia na mashabiki wa Yanga kwa sababu nimekuwa nikishangilia kila nikifunga, hivyo haitakuwa ajabu,” alisema Ajibu.

No comments