Breaking News

Msondo Ngoma waenda kwa Wanasheria, wanataka WCB wawalipe Milioni 300

Ni habari ambazo zimesambaa jioni ya leo kutokana na barua ya Wanasheria iliyosambaa ikionyesha kwamba Band ya Msondo Ngoma inataka kundi la WCB linaloongozwa na Diamond Platnumz liwalipe milioni 300.

Barua hiyo iliyopelekwa pia BASATA naCOSOTA inasema Milioni 300 hizo wanazidai kama fidia kutokana na WCB kutumia bila ruhusa melody ya saxaphone ambayo ni ya wimbo wa Msongo Ngoma.

No comments