Breaking News

Breakng:Mhe. Nape ‘amshambulia’ mdau aliyemuita mnafiki

Mbunge wa jimbo la Mtama, Mhe. Nape Nnauye leo amemjia juu mdau mmoja mtandaoni aliyemuita mtandaoni mnafiki muda mfupi baada ya kuweka posti yake mtandaoni huku akimwambia kuwa mtu huyo ni zaidi ya mchawi.

Mhe. Nape kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika “Usivunje mtungi kwasababu ya panya aliyemo ndani ya mtungi, inamisha taratibu,fanya timing, utaua panya na mtungi utabaki salama!

Baada ya Tweet hiyo mdau mmoja alimjibu kwa kumwambia “mkuu we mnafiki sana yote hayo umeanza baaada ya kuvuliwa uwaziri come on kiongozi bora si yule anaonekana mkosoaji kwa boss“.

Baada ya majibu hayo Mhe. Nape Nnauye alionekana kushindwa kuvumilia kwa kauli hiyo ndipo alipoamua kumjibu mdau huyo kwa kumwambia kuwa vitu anavyovifanya havihusiani na mambo uwaziri na amezoea kufanya hivyo tangia zamani hata kabla ya kuwa waziri enzi hizo alipokuwa Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi.

Wewe ni zaidi ya mchawi, unatumia kamasi badala ya ubongo kuwaza, haya maneno niliyasema nikiwa Mwenezi wa CCM, wakati huo nilikuwa Waziri?“ameandika Mhe. Nape kwa kuhoji.

SOMA NA HII – Hatuwezi kuwa na nchi ya ‘watu wasiojulikana’ – Mhe Nape Nnauye

Mhe. Nape Nnauye ni miongoni mwa Wabunge ambao wanatumia mitandao ya kijamii kuwasilisha mitazamo au maoni yao kwenye jamii.

Soma zaidi-Mhe. Nape afunguka sababu za kuhoji vitu vingi mitandaoni baada ya kuvuliwa uwaziri (+Video)

No comments