Azam FC imetangaza kumuacha staa wake wa kimataifa leo

Club ya Azam FC leo kupitia kwa afisa habari wake Jafari Iddi Maganga imetangaza kumuacha mshambuliaji wao wa kimataifa raia wa Ghana Yahaya Mohamed, Azam FCimefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Yahaya Mohamed baada ya kushindwa kuonesha uwezo mkubwa.

Afisa habari wa Azam FC Jafari Iddi Maganga aliongea na vyombo vya habari leo na kuthibitisha kuwa Yahaya Mohamed leo November 7 2017 wanamshughulikia kwa ajili ya kurudi kwao Ghana kuendeleza maisha mengine ya soka.
No comments