WAKONGWE WATAKAO WIKA MSIMU HUU NBA
WAKATI msimu wa Ligi Kuu ya Kikapu Marekani NBA ukianza mashabiki tayari wameshakaa sawa kushuhudia mechi kali ambazo zinatarajiwa kupigwa. NBA ndiyo ligi maarufu zaidi ya kikapu duniani ikiwa inawashirikisha mastaa wakubwa wengi kutoka sehemu zote kubwa duniani.
Wakati ligi hii ambayo imeanza rasmi jana, kuna wakongwe wanatarajiwa kuwika sana kwenye ligi hiyo na hawa ni baadhi yao: Vince Carter (Sacramento Kings): Unaweza kumuita ‘Air Canada’. Jina ambalo limekuwa likimtambulisha kwenye ulimwengu wa mchezo wa kikapu duniani.
Huu utakuwa msimu wa 20 wa staa huyo wa Kings kwenye NBA, na bado anatarajiwa kuwa anaweza kufanya mambo makubwa sana. Carter amewahi kutajwa kwenye kikosi cha All-Star mara tisa na amekuwa kwenye kikosi bora cha NBA mara mbili. Alifanikiwa kucheza michezo 73 msimu uliopita na kuwa na wastani wa pointi 8.0 rebaundi
No comments